From Wikipedia, the free encyclopedia
Kodi (pia: ushuru) ni malipo ambayo watu wanatozwa na serikali.
Kodi ni chanzo kuu cha mapato kwa serikali ya kisasa. Mapato haya yanagharamia shughuli za serikali, mishahara na marupurupu za watumishi wa dola, gharama za huduma zinazotolewa na serikali au za shughuli za umma: kwa mfano shule, hospitali, ujenzi wa barabara, polisi, mahakama au jeshi.
Kuna njia mbalimbali za kutoza kodi
Siku hizi kodi hutozwa kama pesa lakini kihistoria na katika mazingira ambako watu hawana pesa taslim kodi inatolewa pia kwa njia ya kazi. Mfano ni ujenzi wa barabara ambako wananchi wote wa eneo fulai wanapswa kushiriki na kuchangia kazi yao kwa muda fulani.
Katika mazingira ya mashambani zamani kodi ililipwa pia kwa kutozwa asilimia ya mavuno au mifugo.
Malipo ya kodi ni wajibu wa wananchi hata kama watu wengi wanajaribu kuepukana nayo. Serikali inadai malipo ikitisha adhabu kwa watu wanaoficha mapato yao au wanaokataa malipo.
Serikali huwa na idara za kodi ambazo zimekabidhiwa jukumu la kutunza kumbukumbu ya malipo na kukusanya pesa zinazodaiwa.
Katika mazingira ya kisasa ni makampuni yanayopaswa kukusanya kodi za wafanyakazi kwa njia ya kukata kodi kwenye mshahara na kuzikabidhi kwa serikali.
Biashara zinatakiwa kutunza kumbukumbu za mapato kwa kodi isipokuwa mara nyingi biashara ndogondogo hutozwa kiasi fulani isiyobadilika bila kuchunguza mapato yenyewe.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kodi (ushuru) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.