From Wikipedia, the free encyclopedia
Songea ni manisipaa nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma yenye postikodi namba 57100. Eneo la mji ni wilaya ya Songea Mjini.
Songea | |
Mahali pa mji wa Songea katika Tanzania |
|
Majiranukta: 10°40′48″S 35°39′0″E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Ruvuma |
Wilaya | Songea Mjini |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 126,449 |
Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 131,336 [1].
Kuna barabara ya lami kutoka Songea kupitia Njombe hadi barabara kuu ya Dar es Salaam - Mbeya; pia nyingine ya kwenda pwani kupitia Tunduru na Masasi.
Mji uko kwenye kimo cha m 1210 juu ya UB katika nchi ya Ungoni kwenye nyanda za juu za kusini za Tanzania. Chanzo cha mto Ruvuma kipo karibu na mji.
Jina la Songea ni kumbukumbu ya chifu Songea wa Wangoni aliyekuwa na ikulu yake hapa wakati wa kuenea kwa ukoloni wa Ujerumani akauawa na Wajerumani wa kati wa vita ya majimaji.
Mji wa Songea (iliyoandikwa Ssongea wakati ule) ulianzishwa mwaka 1897 kama kituo cha kijeshi cha Kijerumani. Ukakua kuwa makao makuu ya utawala wa mkoa Songea wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.
Mazingira ya mji yaliathiriwa vibaya na vita ya majimaji na ukandamizaji wake na Wajerumani.
Songea ikaendelea kuwa makao makuu ya mkoa wakati wa utawala wa Uingereza katika Tanganyika na baada ya uhuru katika Tanzania huria.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.