From Wikipedia, the free encyclopedia
Nabii Hagai (kwa Kiebrania חַגַּי, Ḥaggay au "Hag-i", yaani Sikukuu yangu; kwa Kigiriki: Ἀγγαῖος; kwa Kilatini Aggeus) ni mmojawapo kati ya manabii wa Israeli, aliyetoa ujumbe wake miezi ya mwisho ya mwaka 520 KK tu, akihimiza pamoja na nabii Zekaria ujenzi mpya wa hekalu la Yerusalemu baada ya Wayahudi kurudi toka uhamisho wa Babeli.
Hatimaye kazi hiyo ilikamilika na hekalu likatabarukiwa mwaka 515 KK.
Kitabu chake ni kati ya Manabii Wadogo 12 wa Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), kwa hiyo pia kinapatikana katika Agano la Kale, sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.
Tangu kale Hagai anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 16 Desemba[1][2] lakini pia 29 Desemba, au 4 Julai au 16 Julai au 31 Julai.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.