Mnadhiri
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mnadhiri (kutoka Kiebrania נזיר, nazir, maana yake "aliyewekwa wakfu" au "aliyetengwa"[1][2]) katika Biblia ni mtu mwenye nadhiri iliyoratibiwa na Hes 6:1–21.

Humo tunasikia masharti ya nadhiri:
- Kuepa aina zote za vileo,[3] ikiwa pamoja na siki,[4] na hata kumeza chochote chenye sehemu za zabibu.[5]
- Kutonyoa kabisa.[6]
- Kutotiwa unajisi kwa kugusa maiti, hata kama ni kwa kushiriki mazishi ya ndugu.[7]
Kati ya wanadhiri wa kudumu walio maarufu zaidi kuna Samsoni na Yohane Mbatizaji.
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.