Kungwi ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali za nusufamilia Striginae katika familia Strigidae. Spishi fulani zinaitwa kokoko. Ndege hawa ni wakubwa kuliko bundi na spishi za jenasi Bubo ni miongoni mwa spishi kubwa kabisa za Strigidae.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Funga
Kungwi wana mgongo kwa rangi ya kahawa au kijivu pamoja na madoa meupe, na mbele yao ni nyeupe pamoja na madoa au michirizi nyeusi au kahawia. Spishi nyingi zina vishungi viwili vya manyoya vinavyofanana na masikio
Ndege hawa hula mamalia wadogo na wakubwa kiasi hasa (mpaka paa mdogo) lakini ndege, watambaazi na wadudu pia. Kokoko-walasamaki hula samaki hasa. Huwinda usiku.
Kwa kawaida jike huyataga mayai 2 lakini 1-5 inawezekana. Tago lao ni ardhini, mitini, kwenye miamba iliyojitokeza nje na hata kwenye vishubaka vya madirisha.
- Bubo africanus, Kungwi Madoa (Spotted eagle-owl)
- Bubo ascalaphus, Kungwi-jangwa (Pharaoh eagle-owl)
- Bubo bubo, Kungwi wa Ulaya (Eurasian eagle-owl)
- Bubo b. hispanus, Kungwi wa Hispania (Iberian eagle-owl) - imekwisha sasa katika Afrika
- Bubo capensis, Kungwi Kusi (Cape eagle-owl)
- Bubo cinerascens, Kungwi Kijivu (Greyish eagle-owl)
- Bubo lacteus, Kokoko (Verreaux's eagle-owl)
- Bubo leucostictus, Kungwi wa Akun (Akun eagle-owl}
- Bubo poensis, Kungwi wa Fraser (Fraser's eagle-owl)
- Bubo shelleyi, Kungwi wa Shelley (Shelley's eagle-owl)
- Bubo vosseleri, Kokoko wa Usambara (Usambara eagle-owl)
- Jubula lettii, Kungwi Manyoya-marefu (Maned owl)
- Scotopelia bouvieri au Bubo bouvieri, Kokoko-mlasamaki Michirizi (Vermiculated fishing owl)
- Scotopelia peli au Bubo peli, Kokoko-mlasamaki Madoa (Pel's fishing owl)
- Scotopelia ussheri au Bubo ussheri, Kokoko-mlasamaki Mwekundu (Rufous fishing owl)
- Bubo binagadensis (Mwisho wa Pleistocene ya Binagady, Azerbaijan)
- Bubo florianae (Mwisho wa Miocene}
- Bubo leakeyae (Mwanzo wa Pleistocene ya Tanzania)
- Bubo osvaldoi Cuban Horned Owl, (Mwisho wa Pleistocene ya Kuba)
- Bubo sp. (Mwisho wa Pliocene ya Senèze, Ufaransa)
- Bubo sp. (Mwisho wa Pliocene ya Rębielice Królewskie, Poland)
- Bubo sp. (Mwisho wa Pleistocene ya San Josecito Cavern, Mexiko)
- Pulsatrix arredondoi (Mwisho wa Pleistocene ya Cueva de Paredones, Kuba)
Kungwi-jangwa
Kungwi wa Ulaya
Kungwi kusi
Kungwi kijivu
Kokoko
Kokoko-mlasamaki madoa
Rock eagle-owl
Blakiston's fish owl
Dusky eagle-owl
Lesser horned owl
Spot-bellied eagle-owl
Pilippine eagle-owl
Snowy owl
Barred eagle-owl
Great horned owl
Tawny fish owl
Buffy fish owl
Brown fish owl
Crested owl
Tawny-browed owl
Band-bellied owl
Spectacled owl