From Wikipedia, the free encyclopedia
Sikio ni sehemu ya mwili inayowezesha kusikia sauti. Wanadamu na wanyama mamalia wana masikio mawili kichwani. Wanyama wengine husikia sauti kupitia viungo vingine kama vile buibui kupitia nywele za miguu au samaki kupitia neva ndefu iliyopo chini ya ngozi kando ya mwili.
Sikio la binadamu huwa na sehemu ya nje inayoonekana na sehemu isiyoonekana iliyopo ndani ya fuvu. Usikivu wenyewe hutokea kwenye sehemu ya ndani.
Sehemu ya nje yenye kazi ya kupokea na kukusanya mawimbi ya sauti na kuyaelekeza ndani ya njia ya sikio inayoishia kwenye kiwambo cha sikio ambacho ni ngozi inayotikisishwa na sauti.
Kucheza kwa kiwambo kunasikitisha mifupa sikivu ambayo ni mifupa mitatu midogo inayoungwa nacho na mwendo wa mifupa sikivu unapokelewa na mishipa ya fahamu ya sikio la ndani ukibadilishwa kwa mishtuko ya umeme inayopita kwenye neva hadi ubongo. Chumba cha sikio la kati kimeunganishwa na koromeo kwa njia ya neli ya koromeo.
Sehemu ya kiwambo cha sikio pamoja na chumba nyuma yake penye mifupa sikivu huitwa sikio la kati. Nyuma yake kuna sehemu ya sikio la ndani. Kiungo cha mwili kinachobadilisha mwendo wa mishipa sikivu kuwa alama za neva huitwa komboli.
Pamoja na kupokea sauti, sikio la ndani lina pia kazi ya kutunza uwiano wa mwili likiweza kutofautisha kati ya juu, chini, kulia na kushoto.
Wanyama mbalimbali hutumia masikio pia kwa kupoza mwili. Hivyo tembo anatumia masikio yake kama feni.
Sehemu zote tatu za sikio zinaweza kuathiriwa na magonjwa na maumivu.
Kuna pia matatizo ambayo hayajaelewka vema na wataalamu kama tinnitus ambako mtu anasikia sauti ya kudumu ndani ya sikio hata kama wengine hawawezi kusikia kitu. Tatizo lingine ni upotevu wa usikivu upande mmoja unaotokea hasa kwa watu wanaobanwa na matatizo na shughuli nyingi. Matatizo haya yana upande wa nafsi na majaribio ya tiba huenda sambamba na kumpatia mgonjwa kipindi cha raha na mapumziko pamoja na athari nyingine za kutuliza moyo.
Pia watumiaji wa earphones ni rahisi kuumia sikio ukitumia sauti kubwa.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sikio kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.