Kaunti ya Murang'a

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kaunti ya Murang'a
Remove ads

Kaunti ya Murang'a ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Kuhusu mji, soma Murang'a
Ukweli wa haraka Nchi, Nambari ...
Remove ads

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,056,640 katika eneo la km2 2,524.2, msongamano ukiwa hivyo wa watu 419 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Murang'a.

Remove ads

Jiografia

Thumb
Majira ya joto 2022
Thumb
Reli

Kaunti ya Murang'a imepakana na Nyeri (kaskazini), Embu, Machakos (mashariki), Kiambu (kusini) na Nyandarua (magharibi).

Kaunti hii iko kati ya m 914 na m 3353 juu ya usawa wa bahari wastani. Sehemu za magharibi zimekaribia Milima Aberdare na hivyo kuinuka zaidi. Ina mito kadhaa inayotiririka kutoka vitako vya Milima Aberdare kuelekea magharibi ambapo hutiririsha maji katika Mto Tana.

Murang'a ina vilima na mabonde ambayo huwezesha mito kutiririka. Topografia hii huwa na madhara wakati wa mvua kubwa kwa sababu ya mporomoko wa ardhi.

Udongo wa kaunti hii ni wa volkano ambao una rutuba inayowezesha kilimo. Murang'a huhusika katika kilimo cha kahawa, chai, ng'ombe wa maziwa na miti kama zao la biashara.

Murang'a ina maeneo matatu ya tabianchi:

  • Msitu wa mvua wa tropiki, magharibi karibu na Milima Aberdare
  • Nusutropiki, maeneo ya kati
  • Nusuyabisi, mashariki
Remove ads

Utawala

Kaunti ya Murang'a imegawiwa katika maeneo bunge yafuatayo:

Remove ads

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [2]

  • Murang'a East 110,311
  • Kangema 80,447
  • Mathioya 92,814
  • Kahuro 88,193
  • Murang'a South 184,824
  • Gatanga 187,989
  • Kigumo 136,921
  • Kandara 175,098
    • Aberdare Forest 43

Tazama pia

Marejeo

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads