Kaunti ya Murang'a ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Kuhusu mji, soma Murang'a
Ukweli wa haraka Nchi, Namba ...
Kaunti ya Murang'a
Kaunti
Thumb
Bunge la Kaunti ya Murang'a
Thumb
Nembo ya Serikali
Murang’a County in Kenya.svgThumb
Kaunti ya Murang'a katika Kenya
Nchi Kenya
Namba21
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Kati
Makao MakuuMurang'a
Miji mingineMaragua, Kangema
GavanaMwangi wa Iria
Naibu wa GavanaJames Kamau Maina
SenetaIrungu Kang’ata
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Sabina Wanjiru Chege
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Murang'a
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa35
Maeneo bunge/Kaunti ndogo7
Eneokm2 2 524.2 (sq mi 974.6)
Idadi ya watu1,056,640
Wiani wa idadi ya watu419
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutimurang'a.go.ke
Funga

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,056,640 katika eneo la km2 2,524.2, msongamano ukiwa hivyo wa watu 419 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Murang'a.

Jiografia

Thumb
Majira ya joto 2022
Thumb
Reli

Kaunti ya Murang'a imepakana na Nyeri (kaskazini), Embu, Machakos (mashariki), Kiambu (kusini) na Nyandarua (magharibi).

Kaunti hii iko kati ya m 914 na m 3353 juu ya usawa wa bahari wastani. Sehemu za magharibi zimekaribia Milima Aberdare na hivyo kuinuka zaidi. Ina mito kadhaa inayotiririka kutoka vitako vya Milima Aberdare kuelekea magharibi ambapo hutiririsha maji katika Mto Tana.

Murang'a ina vilima na mabonde ambayo huwezesha mito kutiririka. Topografia hii huwa na madhara wakati wa mvua kubwa kwa sababu ya mporomoko wa ardhi.

Udongo wa kaunti hii ni wa volkano ambao una rutuba inayowezesha kilimo. Murang'a huhusika katika kilimo cha kahawa, chai, ng'ombe wa maziwa na miti kama zao la biashara.

Murang'a ina maeneo matatu ya tabianchi:

  • Msitu wa mvua wa tropiki, magharibi karibu na Milima Aberdare
  • Nusutropiki, maeneo ya kati
  • Nusuyabisi, mashariki

Utawala

Kaunti ya Murang'a imegawiwa katika maeneo bunge yafuatayo:

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [2]

  • Murang'a East 110,311
  • Kangema 80,447
  • Mathioya 92,814
  • Kahuro 88,193
  • Murang'a South 184,824
  • Gatanga 187,989
  • Kigumo 136,921
  • Kandara 175,098
    • Aberdare Forest 43

Tazama pia

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.