Kaunti ya Meru
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kuhusu makao makuu, tazama Meru
Kaunti ya Meru | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kaunti | |||||
Kuro katika Mbuga ya Kitaifa ya Meru | |||||
| |||||
Meru County in Kenya.svg Kaunti ya Meru katika Kenya | |||||
Coordinates: 0°3′N 37°38′E | |||||
Nchi | Kenya | ||||
Namba | 12 | ||||
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 | ||||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Mashariki | ||||
Makao Makuu | Meru | ||||
Miji mingine | Maua, Nkubu | ||||
Gavana | Kiraitu Murungi, EGH | ||||
Naibu wa Gavana | Titus Ntuchiu Mutea | ||||
Seneta | Mithika Linturi | ||||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Kawira Mwangaza | ||||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Meru | ||||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 45 | ||||
Mahakama | Mahakama ya Rufaa, Meru | ||||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 9 | ||||
Eneo | km2 7 006.3 (sq mi 2 705.1) | ||||
Idadi ya watu | 1,545,714 | ||||
Wiani wa idadi ya watu | 221 | ||||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||||
Tovuti | meru.go.ke |
Kaunti ya Meru ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Jina lake limetokana na Wameru ambao ndio jamii kubwa zaidi katika kaunti hii.
Sehemu kubwa ya Meru ina ardhi ya rutuba na mvua ya kutosha. Ni kaunti inayojulikana kwa ukuzaji wa miraa, kama zao la biashara. Hata hivyo, ukulima wa ndizi, mahindi, majani ya chai na maharagwe hufanywa[1].
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,545,714 katika eneo la km2 7,006.3, msongamano ukiwa hivyo wa watu 221 kwa kilometa mraba[2]..
Makao makuu yako Meru.
Kaunti ya Meru inapakana na Kaunti za Nyeri, Laikipia, Tharaka Nithi, Isiolo na Kitui.
Iko katika upande wa mashariki mwa Mlima Kenya. Sehemu ya Mbuga ya Kitaifa ya Mlima Kenya iko katika Meru.
Mvua yenye kufaa pamoja na udongo wa volkano huwezesha kilimo. Sehemu za Imenti zilizo karibu na Mlima Kenya huwa ni baridi kidogo na zenye vilima. Sehemu za Tigania hazina hali za kufaa kulima isipokuwa karibu na Vilima vya Nyambene, ambapo huwa baridi kidogo. Mbuga ya Kitaifa ya Meru iko katika sehemu za Igembe, kaskazini mashariki mwa kaunti[3].
Mito, k.v. Mto Kathita hutoka Mlima Kenya na Vilima vya Nyambene na hutiririsha maji yake ndani ya Mto Tana[4].
Meru ni sehemu ya kati ya uliokuwa Mkoa wa Mashariki nchini Kenya upande wa mashariki-kaskazini wa mlima Kenya.
Eneo la Meru lilijumlishwa hadi 1992 katika wilaya ya Meru iliyogawiwa baadaye kuwa wilaya zifuatazo:
Kaunti ya Meru imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo:
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.