From Wikipedia, the free encyclopedia
John Evans Atta Mills (21 Julai 1944 - 24 Julai 2012)[1] alikuwa Rais wa Ghana kwa kuchaguliwa tarehe 7 Januari 2009, baada ya kumshinda mgombea wa chama tawala Nana Akufo-Addo kwa 50.23% - 49.77% katika uchaguzi wa 2008.[2]
John Atta Mills | |
wa 3 Rais wa Ghana (4th Republic) | |
---|---|
wa 2 Makamu wa Rais wa Ghana (4th Republic) | |
Muda wa Utawala 7 Januari 1997 – 7 Januari 2001 | |
Alikuwa Makamu wa Rais 1997-2001 chini ya Rais Jerry Rawlings, naye akasimama bila mafanikio katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2000 na 2004 kama mgombea wa chama cha National Democratic Congress (NDC).
Mills alizaliwa katika Tarkwa, iliyoko katika Mkoa wa Magharibi wa Ghana.[1] Alielimishwa katika shule ya Achimota ,ambapo yeye alihitimu shahada yake mwaka 1963, na Chuo Kikuu cha Ghana, Legon, ambapo yeye alipewa shahada na cheti taalamu katika sheria mwaka 1967.
Wakati akisoma kiwango cha udaktari katika Sheria kutoka Shule ya Oriental and African Studies (SOAS) katika Chuo Kikuu cha London, Mills alikuwa amechaguliwa kwa ugenini, kama msomi wa Fulbright katika Chuo cha Sheria cha Stanford huko Marekani.[2][3]
Mills alihitimu masomo yake ya udaktari katika SOAS, baada ya kukamilisha makala yake ya Thesis katika eneo la ushuru na maendeleo ya kiuchumi. Kazi ya Mills rasmi ya kufunza ilikuwa kama mhadhili wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Ghana, Legon. Alikaa karibu miaka ishirini na mitano akifunza katika Legon na taasisi nyingine za elimu ya juu, na akapanda cheo kuanzia mhadhili, mhadhili mkuu na Profesa, na ni mjumbe katika bodi na kamati mbalimbali. Zaidi ya hayo, yeye alisafiri kutembelea duniani kote kama mhadhili na profesa katika taasisi ya elimu kama vile LSE, na kufafanua utafiti wake na majarida katika mikutano mbali mbali.[3]
Mills ametunga machapisho kadhaa, kama vile [3]
Yeye ameshikilia nafasi za mtahini katika taasisi kadhaa zenye uhusiano na fedha taasisi nchini Ghana, ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Wahasibu, Taasisi ya wafanyikazi wa Benki, na Tume ya ushuru ya Ghana.[3]
Amechangia katika shirika la Ghana la Hockey, Shirika la kitaifa la Michezo nchini, na klabu ya Accra Hearts of Oak. Yeye anafurahia Hockey na kuogelea ,na huchezea kwa mara timu ya taifa ya Hockey (yeye bado ni mwanachama wa timu ya Hockey Veterans).[3]
Tarehe 21 Desemba 2006, Mills alichaguliwa na NDC kama mgombea wake kwa ajili ya uchaguzi wa rais wa 2008 kwa jumla ya 81.4% (kura 1,362), mbali akishinda wapinzani wake, Ekwow Spio-Garbrah, Alhaji Mahama Iddrisu, na Eddie Annan.[3][4] Mwaka 2008, alichaguliwa kuwa rais wa Ghana, baada ya uchaguzi wa pande tatu.
Mills amehusika katika shughuli na miradi mbalimbali kama vile [3]
Alioa Ernestina Naadu Mills, mkufunzi na ana wana Sam Kofi Mills na Ruby Addo.
Alikuwa rafiki mzuri wa Mchungaji T. B. Joshua, mjini Lagos, na kutembelea kanisa lake mara kwa mara. Alisema kufuatia uzinduzi wake kwamba TB Joshua alitabiri kwamba kutakuwa na uchaguzi wa tatu, matokeo yatatolewa Januari, na ataweza kuibuka mshindi.[5]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.