From Wikipedia, the free encyclopedia
Mchwa ni wadudu wadogo wa oda ya chini Isoptera katika oda Blattodea wanaoishi kwa makoloni makubwa katika vichuguu. Kuna aina ya mchwa ambao huishi ndani ya mbao au miti. Takriban spishi zote hula ubao.
Mchwa | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mchwa wafanya kazi na askari | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Familia 10:
| ||||||||||||||
Kila koloni lina malkia, mfalme, askari na wafanyakazi. Askari na wafanyakazi hawana mabawa lakini malkia na mfalme waliwahi kuwa na mabawa walipokuwa vijana. Mfalme anamtia malkia mbegu na huyu anazaa mayai mengi sana. Askari wanalinda kichuguu na wafanyakazi wanafanya kazi nyingine zote.
Mara kwa mara wafanyakazi wanawapatia majana kadhaa chakula fulani ili wawe wadudu wanaoweza kuzaa. Wadudu hawa wana mabawa na huitwa kumbikumbi.[1]
Utafiti wa hivi karibuni waonyesha mchwa, hasa mchwa wa Jangwa la Sahara, kuwa ndiye mnyama anayestahimili joto zaidi. Spishi hii ya mchwa inaweza kustahimili joto hadi nyuzi 55.1.[2]
Mdudu huyu huishi kwa kushirikiana na kutangamana. Yeye halali kabla hajatafuta chakula cha kutosha na cha kuweka akiba.
Hivyo mchwa wametumika katika hadithi nyingi za kitoto ili kufunza maadili ya bidii na umoja. Kwa kawaida, mchwa hukaa wote pamoja katika koloni.
Mwandishi Aesop pia aliandika kuhusu bidii ya mchwa katika hadithi yake 'The Ant and the Grasshopper'.
Katika maandiko ya Biblia (kitabu cha Methali), waumini wameombwa waige mchwa katika utendakazi na umoja.
Katika kitabu kitakatifu cha Waislamu cha Kurani, Sulemani alisikia mchwa akiwaonya wengine warudi nyumbani wasije wakapondwapondwa.
Hata hivyo, watu wengi huona mchwa kama wasumbufu, haswa anapoishi karibu na majengo ya watu. Mchwa hula mbao na kwa hiyo huharibu milango, samani na maboriti ya nyumba.
Wale wanaoishi ndani ya mbao na kula vifaa vya mbao nyumbani huleta pia tatizo la uchafu kutokana na kinyesi chao.[3] Kwa hiyo, watu wengi hutafuta dawa za kuua wadudu hawa au njia nyingine asili za kuwadhibiti kama vile utumizi wa udongo Diatomaceous au mafuta ya kitunguu saumu zinazoathiri wadudu[4].
Wanaofanya taaluma hiyo kwanza huangalia mchwa ni wa aina gani ili waweze kujua amejificha wapi maana wao hujifinya pahala kwingi.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.