From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigezo:Tfm
Esopi, pia Aesop (kutoka kwa Kigiriki Αἴσωπος, Aisopos), alikuwa mshairi wa Ugiriki wa Kale. Ni maarufu kwa ngano zake. Anasemekana alikuwa mtumwa mwenye asili ya Thrakia ambaye aliishi kutoka karibu 620 KK hadi 560 KK katika Ugiriki ya Kale .
Ngano za Esopi huwa na mafundisho mengi ya kimaadili. Wahusika katika masimulizi yake mara nyingi ni wanyama au vitu vinavyoweza kuongea, kupata usuluhisho wa matatizo mbalimbali na hivyo kuonyesha tabia za kibinadamu.
Kuna ngao na hadithi elfu zilizosemekama alizitunga, ingawa hakuna uhakika kama mwenyewe aliandika kitu chochote au kama alikusanya tu masimulizi yaliyokuwepo tayari.
Hadithi zake maarufu zaidi ziko pamoja na "Simba na Panya" au "Kobe na Sungura". Sungura anataka kushindana na kobe kwa mbio akiwa na uhakika atashinda. Kwa hiyo hajitahidi, anatumia nafasi ya kulala usingizi njiani hadi anaona mwishowe kwamba kobe ni mshindi kwa sababu sungura alijiamini mno.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.