Ziwa Amaramba
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ziwa Amaramba (kwa Kireno: Lago Amaramba) ni ziwa lenye kina kifupi nchini Msumbiji, karibu na mpaka na Malawi. Liko kwenye uwanda wa juu wa Nyasa, upande wa kaskazini wa Ziwa Chiuta. [1]
Ziwa Amaramba | |
---|---|
Mahali pa Maziwa ya Amarambo Chiuta Malombe nchini Malawi | |
Mahali | Msumbiji |
Anwani ya kijiografia | 14°22′39″S 35°55′19″E |
Mito ya kuingia | Ziwa Chiuta |
Mito ya kutoka | mto Lugenda |
Nchi za beseni | Msumbiji, Malawi |
Urefu | km 35 |
Upana | km 1.2 |
Eneo la maji | ha 8350 |
Kina kikubwa | mita 5 |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB | mita 635 |
Maziwa hayo mawili yako karibu na kwenye majira ya ukame kuna mfereji unaoyaunganisha, lakini kwenye masika baada ya mvua nyingi yako kama ziwa moja refu. Maji hutoka katika ziwa Amaramba kwa njia ya Mto Lugenda [2] unaoishia katika Ruvuma inayopeleka maji yake kwenda Bahari Hindi.
Maji ya ziwa Amaramba yanatoka linaunganishwa kila wakati na Mto wa Lugenda, mji wa Ruvuma. [3]
Ziwa Amaramba linaenea kwa hektari 8350. Uso wa maji yake unapatikana kwenye mita 635 juu ya usawa wa bahari. Ziwa huwa na urefu wa kilomita 35 na upana wa wastani wa km 1.5. [4] Upande wa mashariki kuna vilima mbalimbali vinavyoitwa Mitumbi, Mero, Mangombo, Chikalulu na Lipembegwe. [5]
Maji ya ziwa ni chanzo endelevu cha maji safi kwa watu katika mazingira yake kwa matumizi ya kilimo na pia kama njia ya usafiri. Mafuriko yanayotokea kila mwaka huacha matope kwenye ardhi iliyo jirani na hivyo kuongeza rutuba ya mashamba. [6]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.