From Wikipedia, the free encyclopedia
Matope ni mchanganyiko wa maji na udongo ambao unatengeneza ujiuji mzito.
Mara nyingi matope hutokea endapo mvua imenyesha sehemu yenye vumbi au udongo au maji mengi kumwagwa sehemu yenye vumbi kama wakati wa utengenezaji wa barabara.
Ni lazima barabara ichimbwe au kuchongwa kabla ya kuanza kutengenezwa; wakati huo ndipo matope hutokea.
Pia matope hupatikana sana sehemu za mabwawa, madimbwi, maziwa na sehemu nyingine ambazo hukusanya maji mengi kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kama vile mito, chemchemi na mvua.
Udongo wa mfinyanzi ukichanganywa na maji unafaa kutengenezea vitu mbalimbali, hata kujenga nyumba za udongo au za matofali.
Matope, hasa ya moto, yanatumika pia kama tiba ya baridi-yabisi.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Matope kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.