Yosefu Sanchez
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yosefu Sanchez (jina kamili kwa Kihispania: José Sanchez Del Rio; Sahuayo, Michoacán, Mexico, 28 Machi 1913 – Sahuayo, 10 Februari 1928) alikuwa mtoto wa Meksiko ambaye aliteswa na kuuawa bila kesi wakati wa Vita vya Wakristero kama alivyotamani[1][2].
Papa Benedikto XVI alimtangaza mwenye heri tarehe 20 Novemba 2005 halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu mfiadini tarehe 16 Oktoba 2016.