Meksiko
nchi katika Amerika ya Kaskazini / From Wikipedia, the free encyclopedia
Meksiko ni nchi kubwa (km2 1,972,550) inayohesabiwa kijiografia kuwa sehemu ya Amerika ya Kaskazini au pengine ya Amerika ya Kati. Kwa vyovyote kiutamaduni ni sehemu ya Amerika ya Kilatini.
Ukweli wa haraka
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: (hakuna) | |||||
Wimbo wa taifa: Himno Nacional Mexicano | |||||
Mji mkuu | Mji wa Mexiko (Kihisp.: Ciudad de Mexico) 19°03′ N 99°22′ W | ||||
Mji mkubwa nchini | Mji wa Mexiko (Kihisp.: Ciudad de Mexico) | ||||
Lugha rasmi | (hakuna kitaifa) Kihispania (hali halisi) | ||||
Serikali Rais |
Shirikisho la Jamhuri Andrés Manuel López Obrador | ||||
Uhuru Imetangazwa imetambuliwa |
16 Septemba 1810 27 Septemba 1821 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,972,550 km² (ya 15) 2.5% | ||||
Idadi ya watu - 2023 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
129,875,529 (ya 10) 101,879,171 61/km² (ya 142) | ||||
Fedha | Peso (MXN ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-8 to -6) varies (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .mx | ||||
Kodi ya simu | +52
- |
Funga
Imepakana na Marekani upande wa kaskazini. Upande wa kusini majirani ni Guatemala na Belize.
Ina pwani ndefu na bahari za Pasifiki na Ghuba ya Meksiko.
Ina muundo wa shirikisho ya majimbo 32 yanayojitawala.
Meksiko ilikuwa nchi ya staarabu za juu ya Waazteki na Wamaya hadi kuvamiwa na Hispania mnamo mwaka 1521, halafu koloni la Hispania hadi uhuru wa mwaka 1821.
Kwa sasa ni nchi ya 15 kiuchumi duniani, hivyo ni pia mwanachama wa kundi la G20.
Mji mkuu ni Mexico City, ambao katika eneo lake lote una watu zaidi ya milioni 20.