![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/d3/Jehoiachin-Jeconiah.jpg/640px-Jehoiachin-Jeconiah.jpg&w=640&q=50)
Mfalme Yekonia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mfalme Yekonia (kwa Kiebrania יְכָנְיָה, Yekonia, au יְהֹויָכִין, Yehoiakin, pia kifupi Konia) alikuwa mtawala wa ufalme wa Yuda kutoka ukoo wa Daudi.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/d3/Jehoiachin-Jeconiah.jpg/320px-Jehoiachin-Jeconiah.jpg)
Alitawala miezi mitatu tu (9 Desemba 598 KK - 15 Machi 597 KK) baada ya baba yake mfalme Yehoyakimu huku mji wa Yerusalemu ukiwa umezingirwa na jeshi la mfalme Nebukadneza II kutoka Babuloni.
Mji ulipotekwa, aliondolewa madarakani (2Fal 24:17) na kupelekwa uhamishoni alipokaa gerezani miaka 37.
Hatimaye alitolewa na kuwa mgeni wa mfalme wa Babuloni hadi kifo chake (2Fal 25:27): habari hiyo imeandikwa mwishoni mwa kitabu cha pili cha Wafalme kama utangulizi wa ukombozi wa Wayahudi wote.
Kama alivyotabiri nabii Yeremia (Yer 22:28-30), hakuna mzao wake aliyetawala tena.