![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/bd/The_Crossing_of_The_Red_Sea.jpg/640px-The_Crossing_of_The_Red_Sea.jpg&w=640&q=50)
Ukombozi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ukombozi, katika dini nyingi, ni msamaha au ondoleo la dhambi zilizopita na kinga dhidi ya laana na mateso mbalimbali, ya milele au ya muda.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/bd/The_Crossing_of_The_Red_Sea.jpg/640px-The_Crossing_of_The_Red_Sea.jpg)
Kwa kawaida ukombozi unasadikiwa kupatikana kwa njia ya kafara au sadaka fulani.
Kati ya dini zinazofundisha ukombozi, kuna Uhindu, Ubuddha na dini za Abrahamu, hasa Ukristo na Uislamu.
Katika aina kadhaa ya Ubuddha, ukombozi unaweza ukapatikana kwa juhudi za mhusika, anapofaulu kubandukana na tamaa zote.[1]
Katika Uyahudi, ukombozi ni ule ambao Mungu aliwatoa Wanaisraeli kutoka Misri, halafu kutoka Mesopotamia.[2]
Katika teolojia ya Ukristo, ukombozi ni hasa ule uliofanywa na Yesu kwa kulipia dhambi za wote msalabani halafu kufufuka mtukufu.[3][4]Waamini wanashiriki kiibada tukio hilo kwa njia ya ubatizo kwanza, na kwa kushiriki ekaristi maisha yao yote.
Katika Uislamu, ukombozi unafikiwa kwa kutofanya tendo lolote lisilolingana na dini hiyo.[5][6] Muislamu akifanya dhambi anatakiwa kumrudia Mungu kwa toba na matendo mema, kama sala na sadaka.[7][8][9]