wilaya katika Mkoa wa Arusha, Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Wilaya ya Monduli ni kati ya wilaya saba za Mkoa wa Arusha yenye postikodi 23400.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Monduli ilihesabiwa kuwa 158,929. Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 227,585 [1].
Wilaya hii iko katika kaskazini mashariki ya Tanzania. Imepakana na Kenya upande wa kaskazini, Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Arusha Vijijini upande wa mashariki, Mkoa wa Manyara upande wa Kusini na Wilaya ya Ngorongoro pamoja na Wilaya ya Karatu upande wa magharibi.
Jina "Monduli" linasemekana kututoka kwa mmoja mzee wa Masai aliyeitwa "Monduli" na kukaa katika eneo la kata ya Monduli Juu wakati wa ukoloni wa Kijerumani.
Wilaya ya Monduli ilikuwa sawa na Jimbo la Uchaguzi la Monduli wakati wa uchaguzi wa bunge. Eneo limegawiwa kwa kata 15 na 51 vijiji au mitaa ya mjini. Eneo lote ni kilomita za mraba 6,419.
Makao makuu ya wilaya iko Monduli Mjini ambayo ni moja wa miji midogo miwili (pamoja na Namanga) katika wilaya yenye tabia ya vijijini.
Monduli iko upande wa magharibi wa Jiji la Arusha na Mlima Meru. Sehemu kubwa ya eneo lake ni milima pamoja na volkeno ya Oldoinyo Lengai iliyokatwa na Bonde la Ufa. Pia mlima karibu na Monduli mjini huitwa Monduli, ni volkeno bwete.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.