Westlife
From Wikipedia, the free encyclopedia
Westlife ni kundi la muziki la nchini Ireland, lililoundwa tarehe 3 Machi 1998.Asili ya kundi hili linajumuisha wanamuziki kama vile Nicky Byrne, Kian Egan, Mark Feehily, Shane Filan na Brian McFadden ambaye ameacha kuimba katika mwaka 2004. Kwa sasa Feehily na Filan ndio wanaotumika kama waimbaji wakuu katika bendi hii. Bendi hii ya Westlife ndiyobendi pekee katika historia ya muziki wa Uingereza kuwahi kuwa na nyimbo za kwanza saba moja kwa moja hadi namba moja, na pia wameweza kuuza hadi nakala zaidi ya milionim arobaini na tano dunia nzima [1]. Ambayo inajumuisha nyimbo zilizorekodiwa studio,video, na albamu zenye kujumuisha nyimbo mbalimbali.[2][3]
Westlife | |
---|---|
![]() Westlife katika tamasha mwaka 2006 | |
Maelezo ya awali | |
Asili yake | Dublin na Sligo, Ireland |
Aina ya muziki | Pop, dance, ballad, pop rock |
Miaka ya kazi | 1998–mpaka sasa |
Studio | Sony BMG, RCA, Syco Music, Aristai |
Tovuti | westlife.com/frontpage |
Wanachama wa sasa | |
Nicky Byrne Kian Egan Mark Feehily Shane Filan | |
Wanachama wa zamani | |
Brian McFadden (1998–2004) |
Walikuwa wanasimamiwa na Simon Cowel na sasa wako chini ya meneja wao ambaye anaitwa Steve Mac. Mwaka 2008, walitangazwa kushika nafasi ya tisa wanamuziki matajiri zaidi walio chini ya umri wa miaka 30, na kushika nafasi ya 13, kwa ujumla. Kwa upande wa Uingereza wamekuwa na nyimbo za peke peke yaani singels hadi kumi na nne, na kushika nafasi ya tatu katika histoia ya Uingereza. Wamewahi kuwa na Cliff Richard na pia wamefanya kazi na Elvis Presley na pia wamewahi kufanya kazi na The Beatles. Kundi hili la muziki limewahi kuvunja rekodi mbalimbali kama vile, Wanamuziki waliowahi, kuwa na miziki mingi katika nafasi ya kwanza nchini Uingereza na pia kwa uuzaji mkubwa zaidi katika eneo la Wembley
Katika miaka mingi ya kazi zao,kundi la Muziki la Westlife wamekuwa wakitengeneza nyimbo za vijana maarufu kama teen pop nyimbo za aina ya pop na kutilia mkazo katika nyimbo aina ya ballads. Wanamuziki wote wanaojumuisha kundi hili ni waandishi wa nyimbo. Lakini nyimbo zao nyingi zimeandikwa na waandishi kutoka nje ya kundi lao. Moja kati ya waandishi maarufu waliowahi kutengeneza nyimbo za kundi hili ni pamoja Steve Mac na Wayne Hector. Tarehe 1/6/2008, Westlife walifanya maadhimisho ya miaka 10, ambapo walifanya tamasha katika jiji la Dublin katika eneo la Croke Park na ambapo watu zaidi ya 83,000 walihudhuria hafla hiyo maalumu. Na kubainisha katika tovuti yao kuwa Westlife walitangazwa rasmi kuwa ndio waliofanya tamasha kubwa zaidi ndani ya miaka 2005 hadi 2008,na kuwa katika nafasi ya saba katika matamasha ya nje ya nchi kwa mwaka 2008.