Waniloti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Waniloti ni watu wenye asili ya bonde la mto Nile[1] ambao wanatumia lugha za Kiniloti, kama vile Wajaluo, Wasara, Wamasai, Wakalenjin, Wadinka, Wanuer, Washilluk, Waateker n.k.
Wanajulikana kwa urefu na weusi wao.
Pamoja na kuwa wengi kati ya wakazi wa Sudan Kusini, wanapatikana pia Ethiopia, Uganda, Kenya na Tanzania[2][3].
Waserer wa Afrika Magharibi pia wana asili hiyo.
Upande wa dini, siku hizi walio wengi wanafuata Ukristo, wakizidi kuacha Dini asilia za Kiafrika.