![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/96/Vitus_CXXVr.jpg/640px-Vitus_CXXVr.jpg&w=640&q=50)
Vitus Mtakatifu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Vitus Mtakatifu alikuwa mtoto Mkristo (labda kutoka Sicilia, kisiwa kikubwa cha Italia) aliyefia dini yake wakati wa dhuluma za makaisari wa Dola la Roma Diocletian na Maximian mwaka 303, akiwa na umri wa miaka 13 hivi[1].
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/96/Vitus_CXXVr.jpg/320px-Vitus_CXXVr.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/19/Vitusmodestuscrescentia.jpg/320px-Vitusmodestuscrescentia.jpg)
Kwa sababu hiyo tangu kale Vitus peke yake, baadaye pamoja na walezi wake Modesto na Kreshensya[2][3], anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Juni[4] ambayo kwa Waorthodoksi ni tarehe 28 Juni ya kalenda ya kimataifa.