![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/8f/Martyrdom_of_Wiborada.jpg/640px-Martyrdom_of_Wiborada.jpg&w=640&q=50)
Viborada
From Wikipedia, the free encyclopedia
Viborada (pia: Wiborada, Guiborat, Weibrath au Viborata; Aargau, leo nchini Uswisi, karne ya 9 – St. Gallen, Uswisi, 1 Mei 926) alikuwa bikira mkaapweke mwenye karama za pekee ambaye hatimaye aliuawa na Wahungari Wapagani kwa sababu ya imani yake na ya maisha yake ya kitawa[1].
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/1b/Wiborada1430.jpg/640px-Wiborada1430.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/8f/Martyrdom_of_Wiborada.jpg/640px-Martyrdom_of_Wiborada.jpg)
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Tena ndiye wa kwanza kutangazwa na Papa. Hilo lilifanywa na Papa Klementi II mwaka 1047.