Papa Klementi II
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Klementi II (1005 – 9 Oktoba 1047) alikuwa Papa kuanzia tarehe 24 Desemba 1046 hadi kifo chake[1]. Alitokea Saksonia, Ujerumani[2].
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e9/Pope_clement_II.jpg/220px-Pope_clement_II.jpg)
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Suidger wa Morsleben und Hornburg. Alichaguliwa kwenye sinodi ya Sutri iliyoitishwa na mfalme Heinrich III wa Ujerumani wakati kulikuwa na watu watatu waliowahi kuchaguliwa kuwa Papa na maaskofu tofauti. Sinodi iliwaondoa wote watatu na kumchagua askofu Mjerumani Suidger ambaye alichukua jina la Kipapa Klementi II.
Alimfuata Papa Gregori VI akafuatwa na Papa Benedikto IX.