nchi katika Ulaya ya Kati From Wikipedia, the free encyclopedia
Uswisi ni nchi ya Ulaya isiyo na pwani katika bahari yoyote.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Kilatini: Unus pro omnibus, omnes pro uno (Kiswahili: "Mmoja kwa ajili ya wote - wote kwa ajili ya mmoja") | |||||
Wimbo wa taifa: Zaburi ya Uswisi | |||||
Mji mkuu | Bern (mji mkuu wa shirikisho) | ||||
Mji mkubwa nchini | Zürich | ||||
Lugha rasmi | Kijerumani, Kifaransa, Kiitalia, Kirumanj[1] | ||||
Serikali Halmashauri ya Shirikisho kwa jumla ni Mkuu wa Dola Mwenyekiti wa mawaziri ana cheo cha "Rais" akibadilika kila mwaka |
Demokrasia, Shirikisho la Jamhuri Viola Amherd (Rais wa Shirikisho mwaka 2024) Karin Keller-Sutter (VP) Guy Parmelin Ignazio Cassis Albert Rösti Elisabeth Baume-Schneider Beat Jans | ||||
Uhuru Imetangazwa Imekubaliwa Shirikisho la Jamhuri |
1 Agosti 1291 1648 1848 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
41,285 km² (ya 132) 4.2 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2019 kadirio - 2013 sensa - Msongamano wa watu |
8,570,146 (ya 99) 8,139,600 207/km² (ya 48) | ||||
Fedha | Swiss franc (CHF ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .ch | ||||
Kodi ya simu | +41
- |
Imepakana na Ujerumani, Ufaransa, Italia, Austria na Liechtenstein.
Jina rasmi ni Confoederatio Helvetica (kwa Kilatini: Shirikisho la Kiswisi).
Majimbo yake 26, ambayo huitwa "kantoni", yanajitawala.
Shirikisho la Uswisi lilianza mwaka 1300 hivi kutokana na ushindi vitani dhidi ya Austria na Burgundy.
Uhuru wa shirikisho kutoka Dola Takatifu la Kiroma ulitambuliwa rasmi katika Amani ya Westphalia mwaka 1648.
Uswisi imepata umaarufu hasa kutokana na sababu zifuatazo:
Mji mkuu wa shirikisho ni Bern.
Mji mkubwa ni Zürich wenye benki nyingi.
Mji wa Geneva ni kati ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa; ni pia makao makuu ya kimataifa ya Umoja wa shirika za Msalaba Mwekundu na mashirikia mengine ya kimataifa.
Hata hivyo Uswisi imekuwa kati ya nchi za mwisho kujiunga na UM (2002).
Kuna lugha rasmi 4: Kijerumani (62.8%), Kifaransa (22.9%), Kiitalia (8.2%) na Kirumanj (0.5%). Lakini wengi wanajua na kutumia lugha zaidi ya moja.
Kati ya lugha za kigeni zinazotumika nyumbani, zinaongoza Kiingereza (5%), Kireno (3.8%), Kialbania (3%), Kihispania (2.6%), Kiserbokroatia (2.5%) n.k.
Upande wa dini, kati ya wakazi, 68% ni Wakristo, hasa Wakatoliki (37.2%) na Wakalvini (25%), lakini pia Waorthodoksi (2.3%) na wengineo. 5.1% ni Waislamu (hasa wahamiaji). 24% hawana dini maalumu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.