Ufalme wa Sardinia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ufalme wa Sardinia (kwa Kiitaliaː Regno di Sardegna) ni jina rasmi la nchi ya Ulaya Kusini iliyodumu miaka 1324-1861, hadi rasi ya Italia ilipounganishwa kwa kiasi kikubwa chini ya ukoo wa Savoia uliokuwa umepewa kutawala kisiwa hicho cha Bahari ya Kati (kwa kukiunganisha na mikoa yake mitatu ya Italia bara: Piemonte, Liguria na Valle d'Aosta) tangu mwaka 1720[1].
Miaka hiyo Ufalme wa Sardinia, ukiwa na makao makuu huko Torino, upande wa bara, ulishiriki vita mbalimbali ili kukamilisha umoja wa rasi na kuteka maeneo mengine.