From Wikipedia, the free encyclopedia
Vita ni mapambano baina ya nchi, mataifa au angalau vikundi vikubwa vya watu yanayoendeshwa kwa nguvu ya silaha.
Katika vita kuna pande mbili au zaidi. Husababisha mateso, vifo na kuharibika kwa mali ya watu pamoja na mazingira asilia.
Asili ya vita ilikuwa mapambano kwa silaha kati ya makabila au vijiji mbalimbali. Baada ya kutokea kwa madola ilikuwa zaidi serikali au watawala wa madola walioamua juu ya vita.
Kuna aina tofauti za vita:
Watekelezaji wa vita huitwa askari au wanajeshi. Historia imejua vipindi ambapo wanaume wote wa nchi fulani walitakiwa kushika silaha na kushiriki katika mapigano. Palikuwa pia na vipindi na utamaduni ambapo wapiganaji walikuwa watu wa pekee wenye jukumu hilo ama kwa sababu walipaswa kuwa askari kufuatana na sheria za nchi au kwa sababu walikodiwa kwa kazi hii.
Wanajeshi rasmi huwa chini ya kanuni za vita lakini sehemu kubwa na vita inashirikisha watu wasiofuata kanuni hizo kama wanamgambo hasa katika vita za wenyewe kwa wenyewe.
Wanadamu wametumia akili nyingi kuboresha vifaa vya vita, yaani silaha, na mbinu za vita. Maendeleo ya silaha yamesababisha kupungua kwa idadi ya askari wanaopigana moja kwa moja lakini uharibifu wa silaha umeongezeka.
Silaha za kale zilitegemea nguvu ya mkono wa mtu zikifikia umbali mdogo. Silaha zimebadilika kulenga mahali ambapo ni mbali zaidi na zaidi. Silaha kali za kisasa zina uwezo wa kuharibu nchi yote; jumla ya silaha za nyuklia inatosha kuua uhai wote duniani.
Kutokana na uharibifu mkubwa unaosababishwa na vita palikuwa tena na tena na makubaliano juu ya kanuni za vita. Kanuni hizo hulenga kupunguza hasara inayosababishwa na mapigano. Lakini historia imejaa pia mifano ambapo kanuni hizo zilivunjwa au kupuuzwa.
Katika karne ya 20 mataifa mengi yalipatana mikataba ya kimataifa juu ya kanuni za vita. Chanzo kilikuwa Mapatano ya Geneva baada ya kuundwa kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu mwaka 1863.
Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia nchi nyingi ziliunda Shirikisho la Mataifa kwa shabaha ya kuzuia vita lakini hii ilishindikana baada ya nchi kubwa kama Urusi, Ujerumani na Italia kupuuza maazimio yake. Kuundwa kwa Umoja wa Mataifa kulikuwa jaribio jipya la kuwa na taasisi ya kimataifa yenye uwezo wa kuzuia vita.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.