Totowe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Totowe ni kata ya Wilaya ya Songwe katika Mkoa wa Songwe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 53815.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 6,260 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,643 [2] walioishi humo.
Karibu na Totowe visukuku vya dinosauri viligunduliwa na kutolewa katika miaka 2004-2009. Alipewa jina la Mnyamawamtuka moyowamkia kwa sababu mifupa hiyo ilipatikana katika korongo la mto Mtuka unaopita katika eneo la Totowe[3].