Tiro
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tiro au Turo (kwa Kiarabu صور, Ṣūr, kwa Kigiriki Τύρος, Týros) ni mji wa Lebanoni kusini maarufu katika historia ya kale hasa kwa utajiri uliotokana na biashara yake ya kupitia baharini. Hata leo unategemea sana bandari yake.
Jina la mji linamaanisha "mwamba"[1] na kutokana na mwamba ambao mji umejengwa juu yake hapo awali.
Wakazi walikuwa 117,000 hivi mwaka 2003,[2][3] na kuufanya mji wa nne nchini Lebanoni.[4]
Utalii unavutiwa na magofu ya zamani, kikiwemo kiwanja cha mashindano ya mbio ya farasi cha wakati wa utawala wa Warumi kilichoorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia mwaka 1979.[5].