From Wikipedia, the free encyclopedia
Mama wa Mungu (kwa Kigiriki Θεοτόκος, Theotókos; kwa Kilatini Deipara au Dei genetrix, yaani "Mzaa Mungu") ni sifa kuu ambayo Wakristo wengi wanampatia Bikira Maria mama wa Yesu Kristo.
Mwaka wa liturujia |
---|
Magharibi |
Mashariki |
Kwa kuwa wafuasi wa Yesu wanasadiki kuwa yeye ni Mungu sawa na Baba, wengi wao wanakubali kuwa aliyemzaa kama binadamu anastahili kuitwa Mama wa Mungu.
Sifa hiyo ilianza kutumika katika karne ya 2, labda nchini Misri, ikathibitishwa moja kwa moja na Mtaguso wa Efeso (431) dhidi ya Patriarki Nestori aliyedai anaweza kuitwa tu Mama wa Yesu au Mama wa Kristo.
Mtaguso mkuu huo uliona kwamba Nestori alimgawa Yesu katika nafsi mbili: ya Kimungu na ya kibinadamu. Kumbe imani sahihi inamkiri kwamba nafsi ya Yesu ni ile ya Kimungu tu ambayo ni ya pili katika Utatu Mtakatifu. Hivyo aliyemzaa Yesu kama binadamu (si kama Mungu, jambo ambalo haliwezekani) anastahili kuitwa Mama wa Mungu (upande wa ubinadamu wake alioutwaa kwake).
Kwa namna ya pekee, Maria anapewa sifa hiyo katika sala ya Salamu Maria, iliyo maarufu zaidi kati ya sala za Ukristo wa magharibi kwa mama wa Yesu.
Sikukuu yake inaadhimishwa na Wakatoliki wanaofuata mapokeo ya Kanisa la Roma tarehe 1 Januari, siku ya nane (Oktava) ya Noeli, lakini Wakatoliki wengine wanaiadhimisha siku tofauti, kwa mfano huko Milano ni Jumapili kabla ya Noeli.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mama wa Mungu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.