Serafino wa Sarov
From Wikipedia, the free encyclopedia
Serafino wa Sarov (kwa Kirusi Серафим Саровский, awali aliitwa Prokhor Moshnin (Прохор Мошнин), 19 Julai 1754 au 1759 - 2 Januari 1833) ni kati ya wamonaki maarufu zaidi wa Urusi kutokana na utakatifu wake.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/7/7f/Seraphim_of_Sarov.jpg/200px-Seraphim_of_Sarov.jpg)
Alistawisha mafundisho ya kimonaki kuhusu sala hasa na kujikana akayaeneza kwa walei.
Kwake lengo la maisha ya Kikristo ni kumpata Roho Mtakatifu zaidi na zaidi. Moja kati ya madondoo yake maarufu zaidi ni hili: "Jipatie roho iliyotulia, na maelfu ya watu wataokolewa kandokando yako."
Serafino alitangazwa mtakatifu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Kirusi tarehe 19 Julai 1903. Hata Papa Yohane Paulo II alimzungumzia kwa kukubali sifa hiyo.[1]
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Januari, lakini pia 19 Julai.