Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi (kwa Kirusi: Ру́сская правосла́вная це́рковь|Rússkaya pravoslávnaya tsérkov) ndilo madhehebu kubwa zaidi ya Ukristo wa Mashariki, likiwa na waumini milioni 112, karibu nusu ya idadi ya Waorthodoksi wote duniani[1].
Pia ndilo Kanisa lililopatwa na dhuluma ya serikali iliyoua Wakristo wengi zaidi katika historia ya Kanisa.
Mkuu wake ndiye Patriarki wa Moscow na wa Urusi wote (kwa maana ya Russia, Ukraina[2] n.k.). Kwa sasa ni Kirill I.