Samuel Morse
From Wikipedia, the free encyclopedia
Samuel Finley Breese Morse (Aprili 27, 1791 - Aprili 2, 1872) alikuwa mvumbuzi wa Marekani. Alibuni telegrafu ya kwanza yenye waya mmoja tu. Jina lake hukumbukwa hasa kwa ajili ya kubuni alfabeti ya Morse.
Tangu miaka ya 1700, kulikuwa na aina tofauti za telegrafu zilizotumia nyaya nyingi. Morse alitumia miaka kadhaa kubuni mashine iliyoweza kupeleka ujumbe kwa kutumia waya mmoja tu, alichofaulu mnamo 1836. [1] Morse na msaidizi wake walibuni msimbo au alfabeti iliyoweza kuonyesha herufi zote kwa kutumia nukta na mistari pekee, ambazo ziliweza kutekelezwa kwa kubofya telegrafu.
Uvumbuzi wa Morse uliwezesha mawasiliano ya haraka na watu walio mbali. Hapo nyaya nyingi za telegrafu zilijengwa. Kati ya nyaya za kwanza za telegrafu ulikuwa ule uliojengwa kati ya Washington, DC na Baltimore nchini Marekani mnamo 1844. Kufikia miaka ya 1860, kulikuwa na nyaya za telegrafu kote baina ya miji ya Marekani, na mnamo 1866, waya wa kwanza wa telegrafu ulivuka Bahari ya Atlantiki. [2]