![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/b5/International_Morse_Code.svg/langsw-640px-International_Morse_Code.svg.png&w=640&q=50)
Alfabeti ya Morse
From Wikipedia, the free encyclopedia
Alfabeti ya Morse (msimbo wa Morse) ni namna ya kuwasilisha herufi, namba au alama nyingine kwa kutumia mahadhi.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/b5/International_Morse_Code.svg/320px-International_Morse_Code.svg.png)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/8d/Seaman_send_Morse_code_signals.jpg/640px-Seaman_send_Morse_code_signals.jpg)
Msimbo wa Morse inatumia nukta na mistari, au alama mbili, moja fupi na nyingine ndefu zaidi.
Alfabeti ya Morse imepata jina lake kutoka Samuel Morse, anayekumbukwa kama mbuni wake. Haitumiwi sana leo kama ilivyokuwa katika karne ya 19 na 20. Tangu karne ya 20 teknolojia tofauti zimechukua nafasi yake.
Kuna aina tofauti za msimbo wa Morse kwa nchi tofauti.
Kuna alama tatu tofauti katika msimbo wa Morse; kuna fupi, kawaida huitwa 'dit', ndefu, inayoitwa 'dah', na kituo. Dah ni ndefu mara tatu kuliko "dit", na kituo huwa na urefu sawa na "dit".