![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/thumb/3/36/Mifumo_ya_mwandishi_duniani.png/640px-Mifumo_ya_mwandishi_duniani.png&w=640&q=50)
Alfabeti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Alfabeti ni kiasi cha alama zinazotumiwa kuandika sauti za lugha fulani. Alama hizi hupatikana kama orodha kwa ufuatano uliokubaliwa, kwa mfano katika Kiswahili: "a, b, ch, d, dh, e, f, g, gh, h, i, j, k, kh, l, m, n, ny, ng', o, p, r, s, sh, u, t, th, v,w, y, z".
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/thumb/3/36/Mifumo_ya_mwandishi_duniani.png/640px-Mifumo_ya_mwandishi_duniani.png)
Alfabeti: Kilatini , Kikirili , Kilatini pamoja na Kikirili , Kigiriki , Kigeorgia na Kiarmenia
Abjadi: Kiarabu , Kiarabu pamoja na Kilatini , Kiebrania pamoja na Kiarabu
Abugida: Kihindi ya Kaskazini , Kihindi ya Kusini , Kiethiopia , Kithaana Mwandiko wa kizalendo wa Kanada ,
Alama kwa neno lote na alama za silabi: Alama za neno lote , Mchanganyiko wa alama za maneno na silabi , Mchanganyiko alfabeti na silabi Mchanganyiko alfabeti na silabi
Jina la "alfabeti" hutokana na mwandiko wa Kigiriki ambamo herufi mbili za kwanza ni α "alfa" na β "beta".
Alfabeti ni mtindo wa mwandiko uliosambaa duniani kote. Kwa lugha nyingi imechukua nafasi ya miandiko ya awali.
Alfabeti huonyesha sauti si maneno kamili - hii ni tofauti na mwandiko kama Kichina wenye alama kwa ajili ya neno lote.