Rosa wa Viterbo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Rosa wa Viterbo (Viterbo, leo mkoani Lazio, Italia, 1233 hivi – 6 Machi 1251[1] ) alikuwa msichana maarufu kwa imani yake katika Ukristo aliyejiunga mapema sana na Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/b/b2/Santarosaviterbo.gif)
Baada ya kuishi kama mkaapweke kuanzia umri wa miaka 7, alianza kuhubiri toba na upatanisho hata alipofukuzwa mjini (1250).
Mwaka huohuo, baada ya Papa kuteka tena Viterbo, alirudishwa kutokana na karama zake za uponyaji na unabii, lakini akafariki mapema kutokana na afya yake mbovu toka zamani.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mwenye heri bikira.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Machi[2] au 4 Septemba, siku ambapo maiti wake asiyeoza ardhini alihamishiwa kanisani (1258). Mpaka leo moyo wake ni mzima.