Roko, Alfonso na Yohane
From Wikipedia, the free encyclopedia
Roko, Alfonso na Yohane (walifariki Caaró, leo nchini Brazil, 15 Novemba na 17 Novemba 1628) walikuwa mapadri wa shirika la Yesu ambao walifia imani ya Kikristo wakifanya umisionari kati ya Waindio.
Alfonso na Yohane walitokea Hispania, kumbe Roko alizaliwa Asuncion, katika Paraguay ya leo.
Wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu wafiadini. Kwanza walitangazwa na Papa Pius XI kuwa wenye heri tarehe 28 Januari 1934, halafu watakatifu na Papa Yohane Paulo II tarehe 16 Mei 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 15 Novemba [1].