![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/88/CalixtusI.jpg/640px-CalixtusI.jpg&w=640&q=50)
Papa Callixtus I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Callixtus I alikuwa Papa kuanzia takriban 218 hadi kifodini chake takriban 222[1].
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/88/CalixtusI.jpg/320px-CalixtusI.jpg)
Alimfuata Papa Zefirino akafuatwa na Papa Urbano I.
Aliwahi kuwa mtumwa[2], lakini mwaka 199 Papa Zefirino alimfanya shemasi na mshauri wake mkuu.
Kisha kuchaguliwa kuwa Papa, kwa upole wake alifaulu kuvuta wafuasi wa uzushi na mafarakano mbalimbali, akifundisha kwamba Kanisa lina mamlaka ya kusamehe dhambi zote. [3][4] Kutokana na msimamo huo, inasemekana waliokuwa wakali zaidi walimchagua Hipoliti wa Roma kama antipapa wa kwanza.[5]