Papa Zephyrinus
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Zephyrinus alikuwa papa kuanzia takriban 198 hadi kifo chake tarehe 20 Desemba 217/218[1]. Alitokea Roma, Italia.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/f/f9/Saintz05.jpg)
Alimfuata Papa Vikta I akafuatwa na Papa Kalisto I.
Alipambana na aina mbalimbali za uzushi kutetea umungu wa Yesu Kristo[2] .
Pia alitegemeza Wakristo katika dhuluma ya kaisari Setimio Severo (193-211)[3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.