Papa Urban I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Urban I alikuwa Papa kuanzia tarehe 14 Oktoba 222 hadi kifo chake tarehe 23 Mei 230[1]. Alitokea Roma, Italia.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/8/84/A_portrait_of_Pope_Saint_Urban_I.jpg)
Alimfuata Papa Kalisto I akafuatwa na Papa Ponsyano.
Urban I ni Papa wa kwanza ambaye tarehe zake zina hakika ya kihistoria[2]. Inaonekana hakukuwa na dhuluma za serikali wakati wa Upapa wake, lakini alipaswa bado kupambana na farakano la Hipoliti wa Roma[3] pamoja na kuongoza kwa uaminifu Kanisa la Roma miaka minane.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, hasa tarehe 19 Mei, sikukuu yake[4].