Otto wa Bamberg
From Wikipedia, the free encyclopedia
Otto wa Bamberg (1060/1061 – 30 Juni 1139) alikuwa chansela wa Dola Takatifu la Roma[1] , halafu askofu wa Bamberg nchini Ujerumani aliyeinjilisha kwa bidii Pomerania[2] alipoongoa Wapagani 20,000 na miji saba bila kutumia silaha kama ilivyofanywa awali[3].
Kwa maadili yake bora[4], tangu kale alitambuliwa kuwa mtakatifu akatangazwa hivyo na Papa Klementi III (1189).