Mtama
From Wikipedia, the free encyclopedia
Makala hii inataja Mtama kama mmea. Kwa makala ya Mtama kata ya Wilaya ya Lindi Vijijini, tafadhali fungua hapa.
Mtama (Sorghum bicolor) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mtama | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mtama (pia: jaddi; Sorghum bicolor) ni mmea wa familia Poaceae (nyasi) katika ngeli ya monokotiledoni.
Asili yake iko katika Afrika ya Mashariki lakini kilimo chake kimeenea hadi Ulaya ya Kusini, Amerika ya Kati na ya Kaskazini na Asia ya Kusini.
Mbegu za mtama ni nafaka ambazo ni chakula muhimu katika Afrika hasa. Kuna pia majaribio ya kuitumia kama zao la nishati ambako mmea wote huchachuliwa kwa kutengeneza gesi na umeme.
Muundo wa mmea umefanana kiasi na mahindi kwa sababu mabua yake hukua kuwa marefu hadi kimo cha mita tano. Mbegu hukua kama mshikamo.
Matumizi yake ni kwa ajili ya uji, supu, keki, mkate na pombe ya mtama. Majani na mabua yake ni malisho ya mifugo na hutumiwa pia kwa kutandika paa la nyumba.
Kwa jumla kuna aina zaidi ya 30 za mtama zinazolimwa kama chakula. Mtama hustawi vizuri kwenye joto ikivumilia pia ukame. Hivyo ni nafaka muhimu kwenye maeneo yabisi ya Afrika. Katika miaka ya nyuma kilimo chake kiliachwa mara nyingi kwa ajili ya mahindi kwa sababu mahindi huleta mazao makubwa zaidi kwa ekari. Lakini wakati wa ukame mahindi ni hasara na watu hurudi-rudi kwenye kilimo cha mtama.
Mtama ni kundi la mbegu ndogo aina ya mazao ya nafaka au nafaka, yanayolimwa sana duniani kote kwa ajili ya chakula na malisho. Hazina kundi la kitaxonomia, bali ni kundi la kikazi au kilimo. Mafananisho muhimu ni kwamba ni nyasi zenye mbegu ndogo zinazolimwa katika mazingira magumu kama yale yaliyo katika hatari ya ukame. Yamekuwa yakilimwa katika Asia ya Mashariki kwa miaka 10,000.[1]