From Wikipedia, the free encyclopedia
Nyasi ni kundi la mimea inayofunika udongo; nyasi zilizo nyingi si kubwa sana lakini aina kama mianzi hufikia urefu wa miti. Kibiolojia hujumlishwa katika familia ya Poaceae au Gramineae.
Nyasi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nyasi | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusufamilia 12
|
Nyasi nyingi huwa na mizizi mirefu inayoshika ganda la juu la ardhi hivyo kuzuia au kupunguza mmomonyoko wa udongo. Kiekolojia aina za nyasi zimezoea mazingira tofauti kabisa kati ya kanda za joto hadi kanda za baridi sana. Wakati wa baridi au ukame majani juu ya ardhi hukauka hata kupotea kabisa lakini mizizi ina uwezo wa kulala muda mrefu na kusubiri mvua au halijoto ya juu zaidi.
Watu wametumia nyasi kwa shughuli mbalimbali. Nyasi ni muhimu kama lishe ya wanyama kama ng'ombe au kondoo. Wanyamapori wengi wanakula nyasi vilevile. Wakulima wanaweza kuteua aina za nyasi zinazofaa kama lishe ya mifugo na kuzipanda. Kumekuwa sababu mbalimbali toka kwa wanasayansi kuelezea kwa nini binadamu hali nyasi.[1]
Aina kadhaa za nyasi hutoa mbegu zinazoliwa na watu kama nafaka; nyasi hizo za nafaka kama vile mahindi, mpunga au ngano ni kati ya vyakula vya msingi vya binadamu duniani kote. Asilimia 70 ya mimea yote inayopandwa ni nyasi.[2]. Aina nyingine za nyasi hutumika pia kama dawa za aina mbalimbali kwa binadamu na viungo vya chakula au vinywaji kama chai.
Katika mazingira ya mjini nyasi za pekee hutumiwa kufunika ardhi hasa katika maeneo ya bustani yanayokanyagwa na watu wengi wanapenda kukalia kwenye nyasi na kupumzika; aina hizi zinatumiwa pia kwenye viwanja vya michezo. Katika bustani nyasi hukatwa kwa mitambo maalum kuwa fupi ili kupendezesha bustani, tofauti na nyasi za mashambani au sehemu za kulishia wanyama.[3] Nyasi hutumika pia kufunika ardhi nje ya nyumba ili kuipendezesha.
Nyasi hutumika pia kwa ujenzi wa nyumba, mara nyingi maeneo ya vijijini, hasa katika nchi zinazoendelea.
Nyasi-bahari zinafanana na nyasi za kweli za oda Poales lakini zinaainishwa katika oda Alismatales. Pwani ya Afrika ya Mashariki ina spishi 12 katika jenasi 8.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.