From Wikipedia, the free encyclopedia
Mnenia ni kata ya Wilaya ya Kondoa katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania, yenye postikodi namba 41709[1] .
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 13,056 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11528 [3] waishio humo.
Baadhi ya vijiji vya kata ya Mnenia vyenye shule ya msingi ni Mnenia yenyewe, Chungai, Filimo na Bambare. Asilimia kubwa za wakazi wa kata ya Mnenia ni Warangi.
Matamshi ya jina la Mnenia yameleta shida ya kuliandika kwa muda mrefu. Sababu yake kuwa matamshi siyo ni bali n ikifuatiwa na y, ila ny katika alfabeti ya Kiswahili ni sauti nyingine. Ndiyo sababu katika uandishi wa lugha ya Kirangi, jina la kata huandikwa Mʉnéen'ya. Kwa lugha ya Kiswahili wengine huandika Mnen'ya.
Kiuchumi Mnen'ya hujulikana hasa kama soko la vitunguu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.