Milima ya Altai
From Wikipedia, the free encyclopedia
Milima ya Altai ni safu ya milima katika Asia ya Kati na ya Mashariki. Milima mirefu zadi hufikia kimo cha mita 4,500.
Urusi, China, Mongolia, na Kazakhstan zinakutana katika milima hii, ambayo ni chanzo cha mito ya Irtysh na Ob.
Safu hiyo imeungwa na Milima ya Sayan kwenye kaskazini mashariki ikiishia upande wa kusini mashariki katika Jangwa la Gobi.
Wakazi wa eneo lake si wengi wakiwa mchanganyiko wa Warusi, Wakazakhi, Waaltai na Wamongolia.
Uchumi wa eneo hilo unategemea ufugaji wa ng'ombe, farasi na kondoo, pamoja na kilimo, misitu, na uchimbaji madini.
Sehemu ya safu hiyo imeorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia.