Uchimbaji madini
uchimbaji wa madini ya thamani au nyenzo nyingine za kijiolojia kutoka duniani / From Wikipedia, the free encyclopedia
Uchimbaji madini ni kitendo cha kuchimba ardhi kwa ajili ya kupata madini. Kitu chochote ambacho hakiwezi kukuzwa kwa njia ya michakato ya kilimo au kuundwa katika maabara au kiwanda ni lazima kichimbwe. Kile kitendo cha kuchukua madini kutoka ardhini ndicho kinachoitwa uchimbaji madini.
.
Uchimbuaji wa madini ya thamani au vifaa vingine vya kijiolojia kutoka duniani unaweza kufanywa ili kupata madini ya metali au yasiyo metali, kwa mfano: almasi, dhahabu, shaba, makaa ya mawe, chumvi, chuma, mawe, chokaa, choko, mwamba chumvi, potashi, changarawe, udongo, petroli, gesi asilia au hata maji.
Uchimbaji mwingine hufanywa kwa kuondoa uchafu juu ya ardhi. Uchimbaji huu huitwa uchimbaji wa juu ya ardhi. Uchimbaji mwingine hufanywa kwa kuchimba ndani zaidi kwenye ardhi kwenye mashimo ya machimbo ya madini. Aina hii ya uchimbaji huitwa uchimbaji wa ardhini. Lakini kuna baadhi ya madini yanachimbwa kwa njia tofauti kabisa na aina hizi za uchimbaji, mfano machimbo ya madini ya dhahabu.
Mfanyakazi anayechimba madini huitwa mchimba madini. Uchimbaji wa madini wa chini ya ardhi ni wa hatari sana: wachimba madini kila mwaka hufa kwenye ajali hizo, mara nyingi katika nchi maskini. Kifaa muhimu kwa ajili ya kuongeza usalama hutumika ili kupunguza vifo vya wachimba madini.
Kuna baadhi ya miji iliyoanza kwa ajili ya uchimbaji madini na wakazi wa maeneo hayo huwa ndio wanaochimba madini hayo kama ajira.