![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/da/Lanzarote_muddycar.jpg/640px-Lanzarote_muddycar.jpg&w=640&q=50)
Uchafu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Uchafu ni yale yanayosababisha kitu au mtu kukosa usafi. Kwa kawaida ni vitu kama vile vumbi, matope, kinyesi au mabaki ya chakula. Kwa Kiswahili "uchafu" unaweza kumaanisha pia hali ya kukosa usafi wa kimaadili au wa kiroho.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/da/Lanzarote_muddycar.jpg/640px-Lanzarote_muddycar.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e1/Dusty-dirty_PC.jpg/640px-Dusty-dirty_PC.jpg)
Kama mata fulani inatazamwa kuwa "chafu" hutegemea wakati, mahali na utamaduni wa mtazamaji. Kwa mtazamo huo uchafu ni mata inayopatikana mahali pasipotakiwa na wakati usiotakiwa. Kwa mfano:
- ardhi kwenye shamba ni malighafi muhimu yenye thamani, lakini kwenye nguo ardhi hiyohiyo ni uchafu
- mavumbi katika mazingira makavu ni jambo la kawaida, yaani punje ndogo za mata thabiti zinazoweza kusukumwa na upepo na kuelea hewani kwa muda hadi kutelemka tena. Kama mavumbi yanatelemka na kukaa kwenye nguo, nywele za watu, dirishani au kwenye gari huitwa uchafu
- rangi hununuliwa hata kwa bei kubwa ili kuipaka kwenye vyombo, nyumba au samani. Rangi ileile ikitiririka kwenye ngozi au kwenye nguo huwa uchafu