Meinradi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Meinradi (Ujerumani, 797 hivi - Einsiedeln, Uswisi, 861) alikuwa mmonaki padri wa utawa wa Wabenedikto ambaye alikwenda kuishi kama mkaapweke akifuata mifano ya Mababu wa jangwani[1].
Umaarufu wake ulipomvutia umati wa watu, alijitafutia mahali pa upweke mkubwa zaidi kati ya milima inayozunguka ziwa la Zurich. Hatimaye aliuawa na majambazi[2].
Alipofariki pakajengwa baadaye kidogo monasteri kubwa iliyotembelewa na watu wengi[3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Januari[4].