From Wikipedia, the free encyclopedia
Mbawakimia kijani ni wadudu wadogo kiasi wa familia Chrysopidae katika oda Neuroptera (wadudu mabawa-vena) walio na mabawa yanayofanana na kimia. Kama jina lao linavyoonyesha wana rangi ya kijani kwa kawaida, huku mbawakimia kahawia (familia Hemerobiidae) wakiwa kahawia kwa wazi.
Mbawakimia kijani | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Chrysoperla carnea | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nusufamilia 3:
| ||||||||||||||||||
Mbawakimia kijani ni wadudu dhaifu wenye urefu wa mwili wa mm 8 hadi 40 na upana wa mabawa wa mm 10 hadi zaidi ya 65, wakubwa zaidi wakiwa spishi za kitropiki. Kwa kawaida mwili wao huwa kijani kibichi hadi hudhurungi-kijani, na machomzolenzi yanaonekana kuwa ya dhahabu katika spishi nyingi. Mabawa ni mangavu yenye kugeuzwa-geuzwa.rangi kidogo. Baadhi wana vena kijani za mabawa, wengine ruwaza ya mabawa ya rangi ya hudhurungi. Zinaposhughulikiwa spishi za baadhi ya jenasi, kama vile Chrysopa na Cunctochrysa, hutoa harufu mbaya kutoka kwa jozi ya tezi za prothoraksi.
Wapevu wana viwambosikio kwenye matako ya mabawa vinavyowawezesha kusikia vizuri. Baadhi ya spishi za Chrysopa huonyesha [[tabia] ya kukwepa wanaposikia miito ya kiukasauti ya popo. Wakati wa kuruka hufunga mabawa yao (ili kufanya ishara yao ya mwangwi kuwa ndogo) na kushuka chini. Mbawakimia kijani pia hutumia mitetemo ya uso wa chini au ya mwili kama njia ya mawasiliano kati yao, haswa wakati wa uchumba. Spishi zilizo takriban sawa kimofolojia zinaweza pengine kutengwa kwa urahisi zaidi kulingana na ishara zao za kujamiiana. Kwa mfano, Chrysoperla mediterranea wa Ulaya ya Kusini anaonekana takriban sawa na jamaa yake ya kaskazini C. carnea, lakini "nyimbo" zao za uchumba ni tofauti sana. Wana wa spishi moja hawatajibu mitetemo ya wengine[1].
Wapevu hukiakia wakati wa utusitusi au usiku. Hula mbelewele, mbochi na mana kuongezwa na matitiri, vidukari na arithropodi wengine wadogo. Baadhi, hasa Chrysopa, ni mbuai haswa. Wengine hula mbochi na vitu kama hivyo takriban peke yao, na huwa na hamira zinazoishi pamoja katika njia ya mmeng'enyo ili kusaidia kupasuka-pasuka chakula kuwa virutubishi.[2]
Mayai hutagwa usiku, moja moja au kwa vikundi vidogo. Jike mmoja hutoa mayai 100-200, ambayo huwekwa kwenye mimea, kwa kawaida ambapo vidukari hupatikana karibu kwa tele. Kila yai hutundikwa kwenye kikonyo chembamba chenye urefu wa sm 1, kwa kawaida kwenye upande wa chini wa jani. Mara tu akitoka, lava hubambua, kisha hutambaa juu ya kikonyo cha yai ili kujilisha. Lava wana umbo jembamba zaidi lenye nundu kwenye thoraksi au ni wanene wenye nywele ngumu ndefu zinazotoka kando. Nywele hizi hukusanya uchafu na mabaki ya chakula (kutikulo tupu za vidukari haswa) ambayo hupatia kamafleji kwa ndege.
Lava ni mbuai walafi wanaoshambulia wadudu wengi wa saizi inayofaa, haswa wenye miili myororo kama vile vidukari, viwavi, lava wa wadudu wengine, mayai ya wadudu na, ikiwa wako wengi sana, pia kila mmoja. Lava wanaweza pia kuuma binadamu mara kwa mara, labda kwa sababu ya uchokozi au njaa[3]. Kwa hivyo, lava hujulikana kwa lugha ya kawaida kama "simba wa vidukari" au "mbwa mwitu wa vidukari", sawa na simba-sisimizi wanaohusiana. Hisia zao hazikuendelezwa vizuri, isipokuwa kwamba ni nyeti sana kwa kuguswa. Wakitembea kwa njia ovyo-ovyo lava huzungusha kichwa chao kutoka upande mmoja hadi mwingine na wanapopiga kitu kinachoweza kuwa mbuawa lava hukishika. Maxila zao zina uwazi ndani yao, hivyo kuruhusu uto wa mmeng'enyo kuingizwa ndani ya mbuawa ambao unaweza kuyeyusha ogani za kidukari katika sekunde 90. Kulingana na hali ya mazingira badiliko kuwa bungo, ambalo hufanyika kwenye kifukofuko, huchukua muda wa wiki 1-3. Spishi kutoka maeneo ya halijoto ya wastani hupitia majira ya baridi kama hatua kabla bungo, ingawa C. carnea hupitia kama wapevu waliobambua juzijuzi.
Kulingana na spishi na hali ya mazingira, baadhi ya mbawakimia kijani watakula tu vitu 150 vya mawindo katika maisha yao yote, huku wengine hula vidukari 100 katika wiki moja. Kwa hivyo, katika nchi kadhaa, mamilioni ya Chrysopidae walafi kama hawa hukuzwa ili kuuzwa kama wadhibiti wa kibiolojia wa wadudu na matitiri wasumbufu katika kilimo na bustani. Wanasafirishwa kama mayai kwa kuwa, kama ilivyoonyeshwa hapo juu, wako wakali sana na hula wenzao katika visanduku. Mayai husambazwa kati ya mimea iliyoathiriwa ambapo hutoka kwenye mayai na lava hufanya kazi yao muhimu. Walakini, utendaji wao ni tofauti tofauti. Kwa hivyo utafiti zaidi unahitajika ili kuboresha ufanisi wa mbawakimia kijani kama mbinu wa udhibiti wa kibiojia wa wadudu wasumbufu. Spishi ambazo hadi sasa zimevutia utafiti mpana na zinapatikana kwa urahisi mzuri kiasi, ni wana kadhaa wa Chrysoperla pamoja na Mallada signatus. Ni mbuai wa asili wa kifukulile wa Ulaya (Ostrinia nubilalis), nondo ambaye hugharimu sekta ya kilimo ya Marekani zaidi ya dola bilioni 1 kila mwaka kama hasara ya mazao na udhibiti wa wasumbufu[4][5].
Watunza bustani wanaweza kuvutia mbawakimia na kwa hivyo kuhakikisha ugavi wa kutosha wa lava kwa kutumia mimea fulani ya rafiki na kuvumilia magugu yenye manufaa. Mbawakimia huvutiwa hasa na Asteraceae, k.m. kaliopsisi (Coreopsis), kosmosi (Cosmos), alizeti (Helianthus) na mchunga (Sonchus), na Apiaceae kama vile bisari (Anethum) na angelika (Angelica).
|
|
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.