From Wikipedia, the free encyclopedia
Hamira ni dawa ya ungaunga au chengachenga inayowekwa kwenye unga uliokandwa ili uvimbe au uwe mchachu na hatimaye chakula kama mkate, pizza, andazi, kitumbua n.k. kipendeze zaidi. Pia hutumiwa katika mchakato wa kuchachusha wanga kuwa vinywaji vya pombe kama bia. Kumbe divai haihitaji kuongeza hamira katika majimaji yaliyokamuliwa katika zabibu.
Kuna aina nyingi za hamira ambazo zote ni vidubini vidogo. Hadi sasa kuna takriban spishi 1500 zilizotambuliwa. [1][2]
Kuna hamira ambazo zimeleta faida kwa binadamu kutokana na matumizi ya kutengeneza vyakula au kwa utafiti wa kitaalamu. Kuna pia aina ambazo zinaweza kusababisha magonjwa.
Ni hasa spishi moja yenye jina la kisayansi la Saccharomyces cerevisiae inayotumiwa katika utengenezaji wa vyakula na vinywaji. Spishi hii imetumiwa na binadamu tangu miaka elfu kadhaa. Inakula kabohidrati katika wanga na sukari na kutoa gesi ya aboni dioksidi pamoja na ethanoli.
Kwa hiyo chanzo cha mkate uliochachuka na pombe ni kilekile isipokuwa kama kinyunga kinapashwa moto alikoholi (pombe) inapotea, ni gesi tu inayofanya mkate kuwa laini, lakini kama majimaji inaongezwa na mchakato wa kuchachua unaendelea ni pombe inayotokea, ambayo aina yake inategemeana na viungo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.